Lango la Maji / Uvunaji wa Maji ya Mvua / Huduma ya Matumizi Mengi (HMM)

From Akvopedia
< Lango la Maji / Uvunaji wa Maji ya Mvua
Revision as of 04:02, 26 January 2016 by Winona (talk | contribs) (Created page with "{{Language-box|english_link=Water Portal / Rainwater Harvesting / Multiple Use Services (MUS)|french_link=Les Services d’eau à usages multiples (MUS)|spanish_link=Servicios...")

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
English Français Español भारत മലയാളം தமிழ் Swahili 한국어 中國 Indonesia Japanese
Mfumo wa matumizi mengi ya maji nchini Nepali hutoa maji masafi pamoja na umwagiliaji wa tone baada ya tone kwa wakulima, ukiwasaidia kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa. Foto: USAID and Winrock International

Huduma ya matumizi mengi ya maji (HMM) ni mjio wa kiuvumbuzi kwa huduma za maji. Inafungulia fursa mpya za kitega uchumi zenye kupunguza umasikini pamoja na haki ya jinsia katika maeneo ya mjini pamoja na maeneo ya vijijini. Katika mpango wa HMM haja ya matumizi mengi ya watu husika ni kipengele cha kwanza, vivyo hivyo katika ubunifu wa mifumo mipya pamoja na kuendeleza kwao mifumo inayokwishatumika. Katika dunia nzima mifumo ya matumizi ya maji nyumbanii au shambani inatumika kwa namna mbalimbali kama ni halali au siyo halali. Kutokana na kupangia matumizi mengi, maslahi kutoka kwa vitega uchumi katika miundombinu huongezeka. Mifano ni: afya, upungufu wa kazi nyumbani, vyakula vingi zaidi, haki ya mapato na jinsia.


Huduma ya matumizi mengi ni jumlisho la namna za huduma za kudumu zinazoboresha afya na hali zilivyo za kazi.

MAJI, AFYA, KAZI. Mchoro: Winrock International

Kipimo cha shambani/nyumbani HMM: lita 200 kwa kila mtu kila siku.

Maji yanapopatikana karibu na nyumba au sehemu zinazoungana ama kwenye mashamba, watu hutumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani pamoja na matumizi ya kazi. Uhusiano huu wa jarabati baina ya matumizi na kuwepo kwa maji unaelezwa katika ‘ngazi ya matumizi mengi ya maji’. Kusudi la pendekezo hili la kisera ni kuwawezesha watu masikini ‘kupanda ngazi ya maji’ pamoja na kutoa lita 50-200 kwa kila mtu kila siku. Kutokana na kiasi hichi lita 3-5 kwa kila mtu kila siku zitasalimishwa kuwa kunywa. Mapato yatatimiza madeni ya mifumo ya matumizi mengi katika muda wa miaka mitatu. Kipimo cha shambani/nyumbani HMM kinanufaisha wanawake sana hasa wale ambao ni wajibu wao kutafuta na kubeba maji hadi nyumbani. Ndio hao ambao wanasimamizi utoaji maji nyumbani. Watu wengine masikini wa ardhi wanaoishi kwenye mashamba ya wengine wananufaika pia.

Kipimo cha jumuiya HMM: usimamizi wa akiba ya maji iliyo karibu nayo inafungamanika

Sasa HMM inalenga majumuiya kama mahali pa kuingiza huduma za maji. Inajumlisha mahitaji ya maji (nyumbani, umwagiliaji, mifugo, upandaji wa miti, uvuvi, shuguli za biashara, sherehe, mazingira) ikizingatia vyanzo vya maji (mvua, maji juu ya ardhi, maji chini ya ardhi, ardhi iliyolowa maji) kwenye maeneo mengi (mashambani, mibuga, pasipo na kizuizi) Usimamizi huu unaofungamanika ulioko kwenye jumuiya una uwezekano wa kupunguza bei ukidumu zaidi kuliko huduma ya namna moja tu.


Advantages Disadvantages
- Hakuna ubaguzi wa jinsia, kwani mahitaji ya Wanaume pamoja na yale ya wanawake hutimizwa.

- Kuboresha uwezo pamoja na haja ya kulipia kunasaidia kuwekeza miradi ya kiserikali na kuendeleza miradi.
- yanayowekezwa na watu binafsi.
- Kuboresha matumizi ya maji kwa wazo la “matumizi mengi zaidi kutoka kila tone”.
- Kuongeza umiliki kwa kujenga kwenye miradi ya majumuiya yanayofungamanika Kutarajia matumizi yote huku uharibifu, migogoro, au kuachiliwa kwa mradi kunatangulizwa na kuepushwa.
- Kuweka maanani uzuri wa maji pamoja na hatari zote zilizopo, matumizi yote na miradi ya kibinafsi.
- Kukubali mgawo wa maji usio na vificho wenye haki unaolinda mazingira pamoja na ulinzi wa akiba za fedha pamoja na ulinzi wa mahitaji ya kinyumbani na kikazi.

- Miradi ya sekta ya maji kwa kawaida haipangiwi kwa matumizi mengi. Kwa hivyo kupanga upya ili kupata matumizi mengi ni changamoto.

- Wakati mwingine mawazo ya kukuza miradi ya matumizi mengi yanaibuka baada ya mradi wa namna moja umeshapangwa. Mawazo hayo mapya yanapingwa na kutangazwa marufuku yakiwa na kutozwa faini.
- Inabidi kueleza bayana dhamiri ya matumizi mengi ya maji nayo mipango ya matumizi ielezwe bayana na mapema.