Lango la Maji / Uvunaji wa Maji ya Mvua / Huduma ya Matumizi Mengi (HMM)

From Akvopedia
Jump to: navigation, search
English Français Español भारत മലയാളം தமிழ் Swahili 한국어 中國 Indonesia Japanese
Mfumo wa matumizi mengi ya maji nchini Nepali hutoa maji masafi pamoja na umwagiliaji wa tone baada ya tone kwa wakulima, ukiwasaidia kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa. Foto: USAID and Winrock International

Huduma ya matumizi mengi ya maji (HMM) ni mjio wa kiuvumbuzi kwa huduma za maji. Inafungulia fursa mpya za kitega uchumi zenye kupunguza umasikini pamoja na haki ya jinsia katika maeneo ya mjini pamoja na maeneo ya vijijini. Katika mpango wa HMM haja ya matumizi mengi ya watu husika ni kipengele cha kwanza, vivyo hivyo katika ubunifu wa mifumo mipya pamoja na kuendeleza kwao mifumo inayokwishatumika. Katika dunia nzima mifumo ya matumizi ya maji nyumbanii au shambani inatumika kwa namna mbalimbali kama ni halali au siyo halali. Kutokana na kupangia matumizi mengi, maslahi kutoka kwa vitega uchumi katika miundombinu huongezeka. Mifano ni: afya, upungufu wa kazi nyumbani, vyakula vingi zaidi, haki ya mapato na jinsia.


Huduma ya matumizi mengi ni jumlisho la namna za huduma za kudumu zinazoboresha afya na hali zilivyo za kazi.

MAJI, AFYA, KAZI. Mchoro: Winrock International

Kipimo cha shambani/nyumbani HMM: lita 200 kwa kila mtu kila siku.

Maji yanapopatikana karibu na nyumba au sehemu zinazoungana ama kwenye mashamba, watu hutumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani pamoja na matumizi ya kazi. Uhusiano huu wa jarabati baina ya matumizi na kuwepo kwa maji unaelezwa katika ‘ngazi ya matumizi mengi ya maji’. Kusudi la pendekezo hili la kisera ni kuwawezesha watu masikini ‘kupanda ngazi ya maji’ pamoja na kutoa lita 50-200 kwa kila mtu kila siku. Kutokana na kiasi hichi lita 3-5 kwa kila mtu kila siku zitasalimishwa kuwa kunywa. Mapato yatatimiza madeni ya mifumo ya matumizi mengi katika muda wa miaka mitatu. Kipimo cha shambani/nyumbani HMM kinanufaisha wanawake sana hasa wale ambao ni wajibu wao kutafuta na kubeba maji hadi nyumbani. Ndio hao ambao wanasimamizi utoaji maji nyumbani. Watu wengine masikini wa ardhi wanaoishi kwenye mashamba ya wengine wananufaika pia.

Kipimo cha jumuiya HMM: usimamizi wa akiba ya maji iliyo karibu nayo inafungamanika

Sasa HMM inalenga majumuiya kama mahali pa kuingiza huduma za maji. Inajumlisha mahitaji ya maji (nyumbani, umwagiliaji, mifugo, upandaji wa miti, uvuvi, shuguli za biashara, sherehe, mazingira) ikizingatia vyanzo vya maji (mvua, maji juu ya ardhi, maji chini ya ardhi, ardhi iliyolowa maji) kwenye maeneo mengi (mashambani, mibuga, pasipo na kizuizi) Usimamizi huu unaofungamanika ulioko kwenye jumuiya una uwezekano wa kupunguza bei ukidumu zaidi kuliko huduma ya namna moja tu.


Advantages Disadvantages
- Hakuna ubaguzi wa jinsia, kwani mahitaji ya Wanaume pamoja na yale ya wanawake hutimizwa.

- Kuboresha uwezo pamoja na haja ya kulipia kunasaidia kuwekeza miradi ya kiserikali na kuendeleza miradi.
- yanayowekezwa na watu binafsi.
- Kuboresha matumizi ya maji kwa wazo la “matumizi mengi zaidi kutoka kila tone”.
- Kuongeza umiliki kwa kujenga kwenye miradi ya majumuiya yanayofungamanika Kutarajia matumizi yote huku uharibifu, migogoro, au kuachiliwa kwa mradi kunatangulizwa na kuepushwa.
- Kuweka maanani uzuri wa maji pamoja na hatari zote zilizopo, matumizi yote na miradi ya kibinafsi.
- Kukubali mgawo wa maji usio na vificho wenye haki unaolinda mazingira pamoja na ulinzi wa akiba za fedha pamoja na ulinzi wa mahitaji ya kinyumbani na kikazi.

- Miradi ya sekta ya maji kwa kawaida haipangiwi kwa matumizi mengi. Kwa hivyo kupanga upya ili kupata matumizi mengi ni changamoto.

- Wakati mwingine mawazo ya kukuza miradi ya matumizi mengi yanaibuka baada ya mradi wa namna moja umeshapangwa. Mawazo hayo mapya yanapingwa na kutangazwa marufuku yakiwa na kutozwa faini.
- Inabidi kueleza bayana dhamiri ya matumizi mengi ya maji nayo mipango ya matumizi ielezwe bayana na mapema.


Inaonekanaje huduma ya matumizi mengi ya maji?

Mara tu unapowafahamu watu wa jumuiya fulani, mahitaji yao, mapendeleo yao, pamoja na vyanzo vyao, unaweza kuunda huduma ya matumizi mengo inayofungamanika. Ikiwa na sehemu zihimilizazo ubora wa afya na kazi. Je, utaamuaje mchanganyiko namna gani wa teknolojia pamoja na programu za uhimili?

1. Maji: Huduma ya matumizi mengi ya maji haina mwenendo wa kurudiarudia teknolojia fulani katika kuhudumia jumuiya fulani. Uchaguzi wa teknolojia faafu unaweza kuwa muhimu sana katika uundaji wa huduma unaotekeleza mahitaji na kudumu kwa kuwezesha jumuiya kutumia teknolojia ile inayofaa kwa matumizi fulani. Vilevile ni muhimu kuchagua programu faafu ya uhimili (mamlaka, usimamizi, namafunzo) ambayo itawezesha huduma kudumu kwa muda mrefu.


Bonyeza ili ku”zoom”. Jedwali: Winrock International

Sehemu nyeti ya programu za kuhimili ni usimamizi. Shirikiana nao watumizi wa maji katika kuunda mfumo wa usimamizi unaothamani maliasili pamoja na vizuizi vyao. Uchaguzi zengine katika uundaji wa mfumo wa usimamizi ni pamoja na usimamizi wa jumuiya (ukiongozwa na kamati au ujumbe) au kundi la wenyeji, familia au mtu peke yake.

2. Afya: Kwa kuwapatia wanaohudumiwa maji yafaayo kunywewa unaweza kupiga hatua muhimu katika kuboresha afya yao. Kwa uwezo wa rasilimali ya mradi, kuunda ziada ya mashuguli yenye kuboresha afya mifano ni pamoja na (elimusiha, udhibiti afya, na lishe) kunaongeza kabisa athari kwa afya zitokanazo na huduma mpya ya maji. Maarifa yatokanayo na mlolongo wa ukadiri pamoja na matokeo ya Kuunda kwa Huduma za Maji yanaweza kubainisha Mashuguli yepi ya Afya yatakayofaa mradi.


Bonyeza ili ku”zoom”. Jedwali: Winrock International


3. Kazi: Pasi na matatizo kuwapatia wahudumiwa huduma ya matumizi mengi ya maji, hali ilivyo ya kazi itaboreka. Kwa uwezo wa rasilimali ya mradi, kuunda ziada ya Mashuguli yenye Kustawishi Kazi mifano nipamoja na (ukulima, ufugaji, biashara) kunaweza kupanua athari ya mradi wako kwa kuongeza mapato na kuwezesha fursa za kujiendeleza kama elimu.


Bonyeza ili ku”zoom”. Jedwali: Winrock International

Ujuzi utokanao kwenyemaeneo ya vijijini

Nchini Nepali, mifumo ya matumizi mengi ya maji ililetwa kwa mara ya kwanza na Nepal Smallholder Market Initiative (SIMI), International Development Enterprise (IDE), na Winrock. Mifumo ni matangi ya kusanya yaliyopo kwenye chemchemi au mito midogo inayogeuzwa kwendea bwawani Iliyoko karibu na kijiji ikisukumwa na mvutano wa ardhi kupitia bomba.

Mifumo hii inahudumia idadi ya familia yapata 10-40 ambayo hutumia maji kwa matumizi nyumbani pamoja na yale ya kilimo cha bustani. Uletaji wa mifumo ya umwagiliaji wa tone baada ya tone ulithibitisha matumizi madhubuti ya maji pamoja na ustawishi bora wa mimea. Asilimia sitini ya watumiaji wa mifumo ya umwagiliaji wa tone baada ya tone hutumia maji yanayopatikana pa karibu nyumbani.

Mradi wa RSR

Akvorsr logo lite.png
Mradi wa 555
WASH Media Forum

Vitabu vya Mwongozo, video na viungo

IDE Nepal, Multiple Use
Water System (MUS) Program
Small scale irrigation
with a rope pump
Rainsong
video

Shukran